Mkoa wa Tabora chimbuko lake ni mji wa Tabora ambao ulianzishwa katika nusu ya kwanza ya karne ya 19 na wafanyabiashara Wakiarabu na Waswahili kutoka Zanzibar. Waliutumia mji huu kama kituo cha njia ya biashara kati ya Pwani na Ziwa Tanganyika. Biashara kuu ilikuwa ya pembe za Ndovu na Utumwa. Mji wa Tabora ulijengwa kwa nyumba za miti na udongo pamoja na ghala za bidhaa kwa ajili ya biashara. Familia ya Tippu Tip ilikuwa kati ya wenye nyumba za mji wa Tabora.
Mwaka 1871 lilishambuliwa Jeshi na la Rugaruga Wajerumani mji wa Mtemi kuharibiwa Mirambo kwa kiasi kikubwa, lakini haikuchukuwa miaka mingi, mji huu ukajengwa upya. Wajerumani walipowasili Tabora waliwakuta wanyamwezi(kabila) kubwa likiwa na tawala mbalimbali za kitemi a (chiefdoms).
CHANZO: TAARIFA YA MIAKA HAMSINI (50) YA UHURU WA TANZANIA BARA
MKOA WA TABORA
Bofya hapa kupakua taarifa yote....
0 comments
Post a Comment