TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDO



Tuesday, March 27, 2012

Chocolate kukufanya mwembamba

Watu wanaokula Chocolate mara kwa mara huwa wembamba. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya. Karibu watu 1000 nchini Marekani walifanyiwa utafiti ambao wamekuwa makini katika vyakula vyao.
Waliokuwa wakila Chocolate mara kwa mara walipatikana wakiwa wembamba kuliko wenzao ambao hula Chocolate baada ya muda.Wanasayansi wanasema, japo Chocolate ina sukari nyingi, ina viungo ambavyo husaidia kupunguza uzito wa mwili, lakini siyo kuchoma mafuta.
Hii siyo mara ya kwanza wanasayansi wameelezea umuhimu wa Chocolate. Utafiti wa awali umeonyesha Chocolate inasaidia moyo.Baadhi ya chocolate zinasaidia kupunguza msukumo wa damu, kiwango cha sukari mwilini pamoja na mafuta.
Lakini kuna onyo la kuwa maakini na Chocolate unayoila kwani baadhi zina sukari na mafuta mengi.Ikiwa unataka kuwa na afya bora, jaribu kula mboga na matunda mengi

Chanzo: BBC SWAHILI

0 comments

Post a Comment