TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDO



Thursday, March 29, 2012

Rhino, Polisi Dar kufungua Daraja la Kwanza Machi 31

TIMU za Rhino Rangers ya Tabora na Polisi Dar es Salaam, zinatarajiwa kuumana Machi 31 mwaka huu, katika moja ya mechi za ufunguzi wa fainali za Ligi Daraja la Kwanza zitakazochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema jana kwamba kila siku zitachezwa mechi mbili, moja ikianza saa 8 mchana wakati ya pili ni saa 10 jioni, ambapo fainali hiyo itamalizika Aprili 22 mwaka huu kwa timu tatu za kwanza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao wa 2012/13.
Alisema mkoa wa Morogoro, umepewa uenyeji baada ya kulipa sh milioni 20.5 kati ya sh milioni 25 zilizotakiwa. Sh milioni 4.5 zilizobakia imekubaliana na (TFF) kuwa itazilipa moja kwa moja kwenye huduma zitakazotumiwa na wasimamizi wa fainali hizo.
Aliongeza kuwa mkoa mwingine uliokuwa umeomba uenyeji ulikuwa Mbeya, lakini hadi kufikia Machi 26 mwaka huu ambayo ilikuwa siku ya mwisho kufanya malipo, ulikuwa umeingiza kwenye akaunti ya TFF sh milioni 15 tu.
Wambura alisema upangaji ratiba ya ligi hiyo ulifanyika juzi kwenye ofisi za TFF na kushuhudiwa na viongozi wa timu saba kati ya tisa zinazocheza fainali hizo, huku mechi ya pili siku ya ufunguzi itakuwa kati ya Trans Camp na Mbeya City Council.
Aprili mosi ni Tanzania Prisons na Polisi Morogoro zitakazocheza mchana wakati jioni ni Mgambo Shooting na Mlale JKT zitapimana ubavu kusaka tiketi ya kucheza Ligi Kuu bara msimu ujao.
“Aprili 2 mwaka huu, ni Polisi Tabora dhidi ya Rhino Rangers (mchana) na Polisi Dar es Salaam itacheza na Trans Camp (jioni). Aprili 3 mwaka huu ni Mbeya City Council itakapoingia dimbani kukipiga na Tanzania Prisons (mchana), huku Polisi Morogoro na Mgambo Shooting zipangwa kucheza jioni,” alisema Wambura.
Wambura aliongeza kuwa Aprili 5, mwaka huu, timu za Polisi Tabora na Mlale JKT zitaonyeshana kazi mchana, wakati jioni Rhino Rangers na Trans Camp zitasaka pointi kwa mara nyingine.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Aprili 6 mwaka huu Polisi Dar es Salaam itacheza na Mbeya City Council mchana, huku Tanzania Prisons na Mgambo Shooting zikijitupa uwanjani jioni.
JKT Mlale, itarudi tena dimbani April 8 mwaka huu kuumana na Polisi Morogoro mchana, huku jioni maafande wa Polisi Tabora na Polisi Dar es Salaam wakitarajia kupimana ubavu. Aprili 9 mwaka huu Mgambo Shooting itacheza na Rhino Rangers mchana na jioni itakuwa zamu ya Trans Camp na Tanzania Prisons.
Aprili 11, Mbeya City Council itachuana na Polisi Tabora mchana na Mlale JKT na Rhino Rangers zikitoana ngeu jioni.

Habari na Tanzania daima

0 comments

Post a Comment