TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDO



Saturday, March 10, 2012

TAARIFA FUPI YA HATUA YA KWANZA YA MPANGO WA KUJITOLEA KUFUNDISHA.

Kama ambavyo asasi ilijipangia  kufanya programu ya kujitolea kufundisha katika likizo fupi iliyopita wiki mbili.
Katika programu hii waliokuwa wakifanya harakati alikuwa ni mhazini wetu  Kiyabo yahaya na katibu wetu wa usajili Mohamed Mapalala, Kwanza napenda niwapongeze na kuwashukuru kwa kutoa muda wao kulisimamia hili kwa ajili ya wanatabora.

HATUA hii imekuwa kama hatua ya kwanza kwani katika mafanikio waliyo yafanya viongozi hawa ni kukutana na afisa elimu wa mkoa na kuitambua asasi na kuwa tayari kufanya utekelezaji wa programu zake haswa zinazogusa suala la elimu. Wamekuwa katika wiki mbili zote hizo wakiwa wanawasiliana na afisa elimu wa mkoa ikiwa wakati mwingine hakuwepo ofisini hivyo kumsubiri amalize ziara zake za kikazi.
HIVYO hatua hiyo imeturahisishie katika zoezi letu hili mwisho wa mwaka kwani muda utakuwa mrefu na hakutakuwa na kikwazo watu watapewa barua za kwenda kwa wakuu wa shule moja kwa moja.
Kama ambavyo nimetoa taarifa awali bado tunaendelea na zoezi la kuandika project TESDO INITIATIVES ON IMPROVING ACADEMIC PERFORMANCE OF SECONDARY SCHOOLS IN TABORA REGION kisha tuombee fedha kwa wadau wa maendeleo ya tabora ikiwapamoja na sisi wenyewe. Mambo yakienda vyema watakao enda kufundisha watawezeshwa kiasi cha kuwapa hali katika utekelezaji.

Na 
Hamisi Masoud Mtwale
Mwenyekiti-TESDO
 

0 comments

Post a Comment