TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDOWednesday, April 25, 2012

RIPOTI KIKAO CHA KAMATI TESDO KILICHOFANYIKA TAREHE 22/04/2012- MDIGRII UDSM-DAR ES SALAAM

 
 
AJENDA
  1. Ufunguzi 
  2. Kujadili, kupitisha na kutafutia pesa project ya elimu shule za sekondari    
  3. Mengineyo

Ufunguzi

Mwenyekiti bwana Hamisi Masoud Mtwale alifungua kikao kwa kumuomba Frank Minazi ambaye ni mjumbe kwa kuomba Mwenyezi Mungu abariki kikao chetu mnamo saa 9 mchana.

Kujadili ,kupitisha na kutafutia pesa mradi wa asasi wa elimu shule za sekondari
Wajumbe wakamati walijadili na kupitisha kufanywa mradi huo kisha kuutafutia pesa ikiwa ni pamoja na kuupeleka kwenye vituo mbalimbali vya redio na kuona watu mabalimbali wenye nia njema na Tabora kwa ajili ya kuchangia. mradi huo unajumuisha kumuisha kuchagua shule 14 za mfano yaani 2 kutoka kila wilaya(Tabora mjini, Nzega, Ulyankulu,Urambo,Igunga,Sikonge,Uyui) ili kusaidia mapungufu yake ya madawati,vitabu na kujitolea kufundisha.masomo yaliyopewa kipaumbele ni physics,chemistry,geography,english,mathematics na biology na kutoa elimu kwa uma kuhusu dhana halisi ya kusoma shule. Pia wajumbe walikubaliana kusomesha wanafunzi 49 wasio na uwezo nao ni 7 kutoka kila wilaya miaka minne yaani kidato cha kwanza -cha nne kwa kulipa ada na kutoa michango ya shule na kuwanunulia sare pamoja na madaftari. Pia katika kujitole akufundisha wajumbe walichangia kuwa watu 84 wenye uwezo wa kufundisha masomo ya kipaumbele wajisajili kwenye fomu yetu iliyopo kwenye blog ,watu hao watapangiwa shule hizo na kupewa hela ya kujikimu kwa miezi miwili. Pia watafanyiwa semina ya siku moja Tabora mjini kabla ya kwenda kufundisha.wakiwa wengu zaidi kipaumbele watapewa wenye fani ya elimu (Education). Bajeti kwa makisio ya mwanzo ilikuwa shilingi 156,759,000.
Mengineyo
Wajumbe waliimizana kuendelea na upendo na mshikamano, na zaidi kupambana kwa halina mali katika kuunusuru mkoa wao wa kihistoria.

Kufunga kikao
Mwenyekiti alifunga kikao hicho mnamo saa 12 jioni kwa kumuomba Mungu awazidishie nguvu, afya na kutekeleza miradi ya asasi.

……………………………………..                                                    …..……………………………..
Hamisi Masoud Mtwale                                                       Mayasa Mzelela Kazala

Mwenyekiti-TESDO                                                             Katibu-TESDO

0 comments

Post a Comment