TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDOMonday, September 3, 2012

USHAURI WA TESDO KUHUSU UPATIKANAJI WA WALIMU KATIKA SHULE ZA SEKONDARI


1.0         Taarifa fupi kuhusu program ya asasi ya kujitolea kufundisha
Awali ya yote tunapenda kuishukuru ofisi yako tukufu kwa kuwa sikivu kwa ushauri lakini pia kuchangia moja kwa moja katika kuhamasisha maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi ya mkoa wetu wa Tabora.
Asasi yetu imeshaanza kufanya jitihada za makusudi katika kunusuru ufaulu duni wa wanafunzi wa mkoa wetu wa tabora na kwa sasa ina kambi darasa kwa ajili ya kutunga mitihani, kufanya masahihisho na kufundisha na kisha kuzifundisha mada ambazo zimeonekana kuwa ngumu kwa watahiniwa katika shule ya Itetemia na Fundikira. Pia tumeombwa na Rwanzari na tumeitikia wito kuiunganisha katika program yetu hii. Tuna walimu 22 tabora mjini na pia tuna walimu wachache Nzega na Uyui.
Pia asasi imeanza program ya kujitolea kufundisha bure (TESDO FREE TUITION) na inafanyia shule ya sekondari Kazima, tunapokea wanfunzi zaidi ya mia tano kila siku.
Mapokezi ya program zetu kwa jamii ya Tabora
Asasi imepata faraja kwa mapokezi mazuri kwa jamii ya watu wa Tabora kuhusu program yetu hii ya kujitolea kufundisha na zaidi tumefurahi shule nyingine kutuomba kufanya program hii katika shule zao mfano mzuri ni shule ya sekondari Rwanzari.

Wanafunzi na walimu wakizungumza kabla ya kuanza vipindi Kazima sekondari ,Tabora mjini

Bofya hapa kupakua taarifa yote

0 comments

Post a Comment