TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDO



Monday, June 4, 2012

RIPOTI YA KIKAO CHA WAJUMBE WA TESDO TAREHE 03/06/2012

RIPOTI YA KIKAO CHA WAJUMBE WA TESDO TAREHE 03/06/2012 DDC MLIMANI PARK saa 10 jioni
AJENDA
  •   Ufunguzi
  •   Mradi wa kujitolea kufundisha
  •   Utafiti wa ufaulu duni wa mkoa wa Tabora,
  •   Uzinduzi wa asasi,
  •   Mengineyo
  •   Kufunga kikao. 
UFUNGUZI

Mwenyekiti alimuomba mjumbe mmoja aombe ili kufungua kikao mnamo saa kumi jioni.

MRADI WA KUJITOLEA KUFUNDISHA

Mwenyekiti alitoa maelezo ya kina kuhusu mradi huo kisha akendelea kutoa sababu au fursa za kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kujengea heshima mkoa, kujijengea heshima mwenyewe na kupata fursa zaidi kama hizi ambazo viongozi wakuu katika mkoa wamekuwa wakitushauri, zaidi wajumbe takribani 20 walijisajili palepale kwa ajili ya programu wakati wengine 25 wakiwa wamejisajili kwenye website, SAUTI MWANZA nao watakuwa na kikao chiniya uongozi wa coordinator wetu JOSEPH MASELE ambaye ni coordinator wa vyuo vyote jiji la Mwanza, na UDOM chini ya Zahoro HM na Malale Buluba, na SAUT TABORA chini ya CASIAN PIUS wanaendelea na usajili huo. wajumbe walipongeza kwa jinsi programu hiyo imepangwa na kuahidi ushiriki wao kwa hali yoyote kuukwamua mkoa wa Tabora na kwa kuanzia itakuwa likizo hii ya mwezi jully kisha walihimiza watu wengine waendele kujisajili il wawepo walimu wa kutosha , na kila mtu wa fani yoyote atapaswa awepo kwenye programu cha msingi tu atapewa semina ya ethics ya taaluma.Zaidi Mwenyekiti alitoa maelezo ya maaumuzi ya kamati kuhusu kuchangia nauli na kutoa t shirt za asasi kwa watakao jiunga na mradi huu wa miezi miwili na kusema kuna kiongozi kaziona jitihada zetu nae ni mkuu wetu wa mkoa FATUMA A. MWASA na kaahidi kutuchangia kuboresha harakati zetu.Wajumbe walimpongeza sana mkuu wa mkoa na kushukuru kwa uongozi wake bora na kumuona kuwa ni mkombozi wa TABORA
UTAFITI WA UFAULU DUNI WA MKOA WA TABORA

Wajumbe waipata maelezo kuwa mkuu wa mkoa ameteua TESDO na SAUT TABORA kufanya tafiti hyo juu na kuja na mpango mkakati wa kuikwamua TABORA wajumbe waliteua kamati ya kulishughulikia hilo ikiwa chini ya Dr. Almas Mabakila (MUHAS) na kupanga kuandaa project hiyo

UZINDUZI WA ASASI

Uzinduzi wa asasi mkoni umekadiliwa kufanywa mwezi wa kumi, na utasimamiwa chini ya kiongozi Frank Jackson
Ernest Minazi

...MENGINEYO

Umoja na mshikamano mpaka tuipate TABORA TUNAYOITAKA
KUFUNGA

Kikao kilifungwa kwa maombi saa 1 kasoro jioni


0 comments

Post a Comment