1.0
Taarifa fupi
kuhusu program ya asasi ya kujitolea kufundisha
Awali ya yote
tunapenda kuishukuru ofisi yako tukufu kwa kuwa sikivu kwa ushauri lakini pia
kuchangia moja kwa moja katika kuhamasisha maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi
ya mkoa wetu wa Tabora.
Asasi yetu
imeshaanza kufanya jitihada za makusudi katika kunusuru ufaulu duni wa
wanafunzi wa mkoa wetu wa tabora na kwa sasa ina kambi darasa kwa ajili ya
kutunga mitihani, kufanya masahihisho na kufundisha na kisha kuzifundisha mada
ambazo zimeonekana kuwa ngumu kwa watahiniwa katika shule ya Itetemia na
Fundikira. Pia tumeombwa na Rwanzari na tumeitikia wito kuiunganisha katika
program yetu hii. Tuna walimu 22 tabora mjini na pia tuna walimu wachache Nzega
na Uyui.
Pia asasi
imeanza program ya kujitolea kufundisha bure (TESDO FREE TUITION) na inafanyia
shule ya sekondari Kazima, tunapokea wanfunzi zaidi ya mia tano kila siku.
Mapokezi ya program zetu kwa jamii ya Tabora
Asasi
imepata faraja kwa mapokezi mazuri kwa jamii ya watu wa Tabora kuhusu program
yetu hii ya kujitolea kufundisha na zaidi tumefurahi shule nyingine kutuomba
kufanya program hii katika shule zao mfano mzuri ni shule ya sekondari
Rwanzari.Wanafunzi na walimu wakizungumza kabla ya kuanza vipindi Kazima sekondari ,Tabora mjini
Bofya hapa kupakua taarifa yote
0 comments
Post a Comment