TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDOWednesday, February 15, 2012

Kauli ya Mwenyekiti TESDO

KAULI YA MWENYEKITI

TURUDI NYUMBANI TULIPO SIO KWETU

Habari zenu ndugu zangu, ndugu wa asili yangu, niwapendao kwa dhati ya moyo wangu.
Ni wazi kwamba tupo sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi yetu hasa tukitafuta mahitaji yetu na pia ikiwa ni sehemu ya ajira zetu, lazima ukisoma kichwa cha habari utashtuka,kwanini jamaaa amesema turudi nyumbani kwetu.
Binafsi naamini kuna njia mbili za kufika mahali
  • Kimwili
  • Kifikra
na ninaposema sema turudi nyumbani haswa namaanisha kutumia njia hizo, ni wazi kati yetu huwa tunaonavigumu kujitaja mbele za watu tunatokea TABORA na kusema hivyo tunaona ni kitendo cha aibu kwanza mkoa upo nyuma kimaendeleo ikiwa kauli yetu kubwa.
Kwa muda mrefu sasa wasomi, wajasiliamali wakubwa , watu wenye mafanikio, watu wa kawaida na kada mbalmbali kutoka mkoa wa Tabora wamekuwa kimya katika kutoa eidha michango yao ya fikra au ya mali katika kuhamasisha maendeleo ya mkoa wetu.TESDO tunaona sasa ni wakati muafaka wakutoa fikra zetu duni na kuungana katika asasi yetu hii kwani lazima tujue tuna uwezo wa kuchangia katika yale tunayoona ni changamoto za mkoa wetu. WAHENGA WANASEMA MKATAA KWAO MTUMWA.
Ni kweli tulipasahau kwetu, ni kweli tulijivunia sehemu za wenzetu leo tumebaini na kukubali kwa dhati ya moyo wetu na zaidi tunaamini KUTELEZA SI KUANGUKA,
Tutasimama imara kwa kila hali tutajitoa kwa fikra zetu, mali zetu..TESDO TUNAOMBA KILA MTU AICHUKUE KAULI HII NA AIWEKE MOYONI MWAKE KIUTEKELEZAJI.
Sasa tumeisha peleka maombi yetu CRDB ya kufungua akaunti ya asasi na tumeahidiwa twende leo(tar 15/02/2012)
Baada ya hapo kila atakae chukua fomu ya usajili kwa mapenzi yake na mkoa wetu atairuridisha akiwa kalipa gharama za usajili kwenye akaunti ya asasi.
Mungu wetu tulipatenga kwetu na kutukuza kwingine sasa tumekumbuka ni jukumu letu kupapenda kwetu kwani tumelelewa hadi tukapata mafanikio haya SASA TUMEAMUA KURUDI NYUMBANI HUKU TULIPO SIO KWETU

Na Hamisi Masoud Mtwale 
Mwenyekiti-TESDO

TESDO NI YETU, TABORA NI YETU NA MAFANIKIO YAKE NI YETU PIA

0 comments

Post a Comment