TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDO



Thursday, March 8, 2012

RC -Tumbaku ikipewa kipaumbele, bangi iruhusiwe.

SERIKALI mkoani Singida imesema zao la tumbaku haliwezi kuwekwa kwenye orodha ya mazao ya kipaumbele ya mkoa wala wilaya kwa kuwa zao hilo lina hasara nyingi kuliko faida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, aliyasema hayo juzi mjini hapa wakati wa hafla ya kukabidhi matrekta saba kwa vyama vya ushirika vya msingi vya Masgati, Mitundu, Makale Itagata, Kintanula, Mwamagembe na Rungwa katika Wilaya ya Manyoni.

Dk. Kone alikuwa akijibu risala ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Kati (CETCU Ltd) iliyosomwa na Mwenyekiti wao, Hamisi Mwanjowa, ambapo ilisema moja ya changamoto inayokabili chama hicho ni mkoa kutolipa kipaumbele zao la tumbaku.

Risala iliendelea kufafanua kuwa kitendo cha mkoa au wilaya kutoliweka zao hilo kwenye orodha ya mazao ya kipaumbele, imesababisha kukosekana kwa nguvu ya pamoja katika kuhimiza uzalishaji wa tumbaku katika eneo hilo.

Akionesha dhahiri kukerwa na maelezo hayo, Dk. Kone alisema mkoa hauko tayari kulipigia upatu zao hilo kwa kuwa tumbaku ni zao choyo na lina hasara nyingi kuliko faida.

“Tumbaku ni zao choyo….lakini alizeti na pamba ni mazao rafiki. Kama utaniambia niipe tumbaku kipaumbele, basi hata bangi niruhusu ilimwe” alisema Mkuu huyo wa Mkoa na kuongeza “hatuwezi kutoa kipaumbele kwa tumbaku, dhamira yangu hainiruhusu.”

Aidha, alionesha kutoridhishwa kwake na utaratibu wa kununua matrekta hayo kutoka nje ya nchi moja kwa moja akisema kuwa gharama kubwa ya manunuzi hayo ingeweza kuepukwa kama yangenunuliwa humu nchini.

Awali, Mwenyekiti wa CETCU Ltd, Mwanjowa alijinasibu kuwa Chama hicho cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku kinahudumia vyama vya msingi 14 ambavyo vilizalisha wastani wa kilo 2,039,084.33 sawa na mapato ya Sh bilioni 6.8 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Habari kwa msaada wa Habari Leo

0 comments

Post a Comment