TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDOMonday, March 12, 2012

Manji azindua kampuni mpya ya simu za mkononi

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuf Manji, anatarajia kuzindua Kampuni ya mwasiliano ya MyCell ambayo ni kampuni tanzu ya Quality Group Limited.
Huduma hizo zinatarajiwa kuzundiliwa mkoani Dar es Dar es Salaam siku 15 zijazo kupitia mtandao wa kisasa wa 3.5 G.

Kauli hiyo, imetolewa jana na Mkurugenzi wa Ufundi wa kampuni hiyo, Kanali Anurag Chandra, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam,baada ya ziara ya ukaguzi makao makuu ya Mycell ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Professa Nkoma.

Chandra,alisema mbali ya Dar es Salaam, pia wameanda mipango ya kueneza huduma hizo nchi nzima, hali itakayoifanya kuwa kampuni ya kwanza binafsi inayomilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100 kuendesha shughuli zake kikamilifu katika sekta a mawasiliano.

“Katika hatua za awali soko la Mycell, litalenga wateja wa kitaasisi kama vile benki, kampuni za bima, hospitali, vyuo vikuu, taasisi za taifa za teknolojia ambazo zitanufaika kwa huduma mbalimbali fanisi na uhakika, ikiwamo televisheni kupitia simu ya mkononi, video, mkutano kwa njia ya video, tiba kwa njia ya mtandao (tele-medicine).

Kanali Chandra, alisema kutokana na kuwapo mfumo wa mitandao ya kisasa na iliyosanifiwa vyema, hakutakuwa na msongamano wa mawasiliano na hivyo huduma zake kuwa suluhisho la kudumu kwa shughuli zinazohitaji uharaka kama vile mawasiliano ya kiutawala kwa njia ya mtandao, kukabiliana na majanga,menejimenti, huduma za afya, mfumo wa kisheria, sekta ya elimu na madini.

“Nawahakikishia teknolojia ya mawasiliano ya 3.5G ya Mycell, inatilia mkazo ubora wa huduma ikiwamo ubora wa juu wa sauti, intaneti na huduma nyingine za habari kwa kutumia mtandano imara na wa kisasa,

“Mtandao mkuu uliowekwa una uwezo wa kutoa kasi inayofikia mbp 10 kwa sekunde na kuufanya kuwa mtandao wenye kasi zaidi ukanda huu. Mtandao wa 3.5G, ambao unatokana na teknolojia ya EVDO Rev-A muda mfupi ujao, utaboreshwa kuwa katika teknolojia ya ‘EVDO Rev-B,’ ukitarajia kutoa kasi ya mbp 15 kwa sekunde, na kuifanya MyCell kuwa kampuni ya kwanza barani Afrika kujiunga na teknolojia ya EVDO Rev-B,” alisema.

Habari Mtanzania

0 comments

Post a Comment