TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDOMonday, March 12, 2012

Wanasiasa vinara mauaji ya albino

BAADHI ya wanasiasa na watu wanaosaka uongozi serikalini, wametajwa kuwa ndiyo vinara wakubwa wa mauaji ya walemavu wa ngozi (albino) kwa imani za kishirikina.
Tuhuma hizo nzito zimetolewa juzi na chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoani Kagera (Albino) mbele ya timu ya Tathimini ya Utawala Bora Barani Afrika (APRM).
Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Mkoani Kagera, Burchard Mpaka, aliiambia timu hiyo iliyokutana na wadau wa utawala bora jana mjini Bukoba, ya kuwa mtandao wa wanasiasa na viongozi ndiyo wanaojihusisha kutafuta viungo vya albino.
Kwa mujibu wa Mpaka mbele ya timu hiyo yenye wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali kutoka nchi za Afrika, alidai yameshatokea mauaji saba ya watu wenye ulemavu mkoani Kagera.
“Watoto wenye ulemavu wa ngozi wamebaki kuwa wakimbizi watuhumiwa wakubwa ni wanasiasa, viongozi wanaotafuta madaraka serikalini na wafanyabiashara wa madini. Wanasiasa eti wakipata viungo vya albino wanashinda kura nyingi,” alidai mwenyekiti huyo.
Hata hivyo maelezo ya Mpaka yalimfanya kiongozi wa timu ya APRM mkoani hapa Profesa Aderick Nade kutoka nchini Nigeria, ahoji ni wanasiasa wangapi wamefikishwa mahakama kutokana na tuhuma za kujihusisha na mauaji ya albino.
Washiriki wa mkutano huo walijibu kwa pamoja kuwa hakuna mwanasiasa aliyekamatwa na waliofikishwa mahakamani ni wakulima.
Akizungumza na wadau hao Profesa Nade aliyeongoza timu ya wataalamu tisa waliofika Kagera wakiwa miongoni mwa 21 waliowasili hapa nchini mapema wiki hii, alisema lengo la Mpango wa Tathmini ya Utendaji kwa Nchi za Afrika (APRM) ni kuangalia mwelekeo mpya wa bara hilo na kutafsiri misingi ya utawala bora.
Awali akifungua mkutano huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Nassoro Mnambila, alisema serikali inakabiliwa na changamoto kubwa katika suala la utekelezaji wa misingi ya utawala bora.
Alikiri kuwa miongoni mwa maeneo ambayo serikali haijafanya kwa kiwango cha kuridhisha ni kuendelea kuwepo kwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe na baadhi ya makundi kutoshirikishwa kikamilifu katika masuala ya kisheria.
Hata hivyo Mnambila alisema suala la utawala bora linabeba tafsiri pana katika matumizi bora ya rasilimali zinazotakiwa kuwa chanzo cha huduma bora, kujali haki za binadamu na serikali kuwajibika ipasavyo kwa wananchi walioiweka madarakani.
Hoja zitakazobainishwa na timu ya wataalamu hao kutoka nchi mbalimbali zitawasilishwa katika kikao cha wakuu wa nchi za Afrika kinachotarajiwa kufanyika Julai jijini Lilongwe ambazo zitatolewa majibu na wakuu wa nchi.

Habari na Tanzania Daima

0 comments

Post a Comment