TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDOMonday, March 19, 2012

MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO YA AFYA MWAKA WA MASOMO 2012/13

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anakaribisha maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali
zinazotolewa na Wizara ya Afya kwa mwaka wa masomo 2012/2013.
1.
Kozi zinazotangazwa ni:
A. Kozi za ngazi ya Stashahada:
(i) Afisa Afya ya Mazingira (Health Officer)
(ii) Fiziotherapia (Physiotherapy)
(iii) Fundi Sanifu Meno (Dental Laboratory Technologist)
(iv) Mteknolojia Maabara (Laboratory Technician)
(v) Optometria (Optometry)
(vi) Tabibu (Clinical Officer)
(vii) Tabibu Meno (Dental Therapist)
(viii) Uuguzi Daraja ‘’A’’ (Diploma in Nursing)

Bofya hapa kupakua taarifa yote

0 comments

Post a Comment