TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDO



Saturday, March 17, 2012

TANGAZO KUHUSU NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anatangaza nafasi za mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada kwa
mwaka wa masomo 2012/2013 kama ifuatavyo:
(A) MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI
1.
CHETI DARAJA A: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Aliyehitimu Kidato cha 4 kati ya mwaka 2009 hadi 2011 na kufaulu katika kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 kwa
mtihani uliofanyika katika kikao kimoja AU mwenye ufaulu wa masomo manne kwa kiwango cha C au zaidi (masomo
yanayofundishwa katika shule za Msingi) kwa mitihani iliyofanyika katika vikao zaidi ya kimoja;
(b) Aliyehitimu Kidato cha 6 na kukosa sifa za kujiunga na Stashahada ni sifa ya nyongeza.
Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya ‘Mathematics, Biology, Physics, Chemistry and English‟.
Bofya hapa kupakua taarifa yote

0 comments

Post a Comment