TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDOFriday, March 16, 2012

Namna yakurudisha mafolder yaliyobadilishwa na kirusi nakua shortcut

Mara nyingi hutokea endapo flash disk yako inapokua imeshambuliwa na computer virus. Usipate tabu unaweza kurudisha mafolder yako katika hali yakawaida. Trojan virus anaposhambulia flash disk hubadilisha folders nakua shortcut.. Folders hua namuonekano kama huu hapa
 Kitaalam shortcut folder huwa na jina hili 0x29ACAAD1.exe. Karspersky antivirus huliona folder hilo kama Trojan virus mwenye jina Trojan.Win32.VBKrypt.cvcu.
ONYO: USILIFUNGUE HILO FOLDER KWANI UTAKUA UMEFUNGUA KIRUSI
Fuata maelekezo yafuatayo kurejesha folder lililoathiriwa na kirus:
1.    Fungua START, kasha bofya RUN
2.    Andika “cmd” kasha bofya OK
3.    Itafunguka window ya rangi nyeusi. Andika maneno yafuatayo
                   attrib -h -r -s /s /d f:\*.*

NB: Badilisha  “f” kwa herufi ya flashdisk yako ndani ya computer, inaweza ikawa g,h nk..
          4: Kisha bofya ENTER.
Baada ya hapo utaona mafolder ya aina mbili, yale yenye shortcut na mafolder original. Kopi hayo mafolder original kwenda sehem nyingine ndani ya computer yako.Kisha format flashdisk yako.

Ukipata tatizo lolote usisite kutoa maoni yako hapa chini kwa msaada zaidi...

0 comments

Post a Comment