TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDOWednesday, May 16, 2012

UJUMBE WA TESDO UMEMFIKIA MKUU WA MKOA WA TABORA

Tunamshukuru mungu ujumbe wa TESDO leo umemfikia mkuu wa mkoa wa TABORA, MH. FATUMA A. MWASA.
Awali ya yote tunapenda kumpongeza mama yetu kwa jitihada ambazo anaonyesha katika mkoa wetu zikiwa katika kuhamasisha maendeleo ya uchumi na jamii. Tumemueleza adhma yetu na kwa kuwa ni mdau mkuu wa maendeleo ya mkoa ametuahidi kutuunga mkono na kutuchangia kwa mradi wetu wa elimu (TESDO INITIATIVES FOR IMPROVING PERFOMANCE OF SEC SCHOOLS IN TBR REGION) na zaidi ametushauri katika NYANJA ya uchumi kuhusu miradi miwili ya KILIMO. Mwisho amewapa salam na kuwapongeza kwa kuwa na umoja huu na kuwaomba mjisajili kwa wing katika kujitolea kufundisha na katika asasi. Tena ametualika kwenye kikao kikuu cha kamati ya mkoa jumamosi tar 19/05/2012 tukashiriki na ku present. Pia tumefanikisha kupata ofisi ya makao makuu town centre.
Natoa wito kwa wote kujisajili katika asasi kwa vituo tulivyopangiana na pia kwa programu ya mwezi wa 7 ya kujitolea kufundisha. kwa usajili bofya hapa Fomu ya kujisajili kujitolea kufundisha 
Ni dhahir maendeleo yetu tutayaleta wenyewe kwa kushirikiana na wadau wengine.TESDO NI YETU, TABORA NI YETU NA MAENDELEO YAKE NI YETU PIA

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti

0 comments

Post a Comment