TESDO MAKAO MAKUU TABORA

tesdo makao makuu

Usajili utafanyika kwa vituo vitatu, TABORA,DODOMA na DAR ES SALAAM, unatakiwa kudownload fomu kwenye blog ya asasi na kuijaza vyema, kisha unatakiwa ulipie ada ya uanachama na fomu kama inavyojieleza kwenye hiyo fomu. Akaunti no 01522250952400. Kwa kituo cha TABORA utakabidhi fomu yakokwa Mohamed Mapalala 0715449745, DODOMA Zahoro HM na Malale Buluba 0764492146. DAR ES SALAAM Mayasa Mzelela 0785314908, kasha baada ya muda utapatiwa risiti yako. Fomu inapatikana sehemu ya TESDO DOCUMENTS. Kwa maoni kuhusu utaratibu tuma kwenye email tesdo@rocketmail.com au simu 0716555450/0785314908.

Hamisi Masoud Mtwale

Mwenyekiti TESDO



Saturday, May 5, 2012

Waliofariki ajali ya NBS watambuliwa

MIILI ya watu saba waliofariki dunia katika ajali ya basi la NBS wilayani Igunga Mkoani Tabora juzi zimetambuliwa na ndugu zao ambao tayari wameshaaza taratibu za maziko.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Jiner na kusababisha watu saba kufariki papo hapo na wengine 54 kujeruhiwa huku majeruhi wanne wakisafirishwa kupelekwa katika Hospitali za Rufaa.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Joseph Kisara akizungumuza na waandhishi wa Habari jana alisema kuwa miili ya marehemu sabatayari imetambuliwa na ndugu zao.
Joseph aliyataja majina ya marehemu kuwa ni Dicksoni Nassani, Zainabu Hamudu, Anna Kisima, Msemo Advocatus, Kalekwa Ramadhani ambaye alikuwa na mtoto wake wa kiume na kafariki katika ajari hiyo huku akitambulika kwa jina mmoja la Saidi pamoja na mumoja kufahamika kwa jina la Msukuma wa Mwanza.

Alisema kuwa majeruhi waliopata ruhusa kulingana na haliza ni majeruhi 32 huku majeruhi wanne wakibaki hospitalini hapo kuendelea na matibabu.
Alibainisha kuwa majeruhi wanne wenye hali mbaya wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando kwa matibabu zaidi kulingana na uhaba wa vifaa katika Hospitali hiyo ya Wilaya.
Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Iddi Hussein ambaye ni dereva wa basi hilo, Romana Rabia pamoja na Happy Saidi ambao wote kwa pamoja wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini mwanza kwaa matibabu zaidi.
Aliongeza kuwa majeruhi waote waliopatiwa ruhusa hali zao zinaendelea vizuri na kuongeza kuwa na wale waliolazwa wanaendelea na matibabu.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Antony Lutta alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa matairi ya mbele na kuababisha vifo vya watu saba papo hapo.
Lutta aliongeza kuwa jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa ajili hiyo ilikubaini chanzo chake.

Habari kwa msaada wa mwananchi gazeti

0 comments

Post a Comment