UTANGULIZI
Namshukuru Mungu kwa uwezo aliotupa Viongozi na Wana TESDO wa kuwatumikia vyema wana Tabora.Pia shukrani za dhati ziende kwa watendaji wa CG FM radio,VOT Radio na Mhe.Mstahiki Meya wa Manispaa kwa mchango wake wa TSH.50,000/=.
URATIBU WA SEMINA
Semina ya kuwaelimisha wanafunzi walio maliza kidato cha 6 na 4 iliratibiwa chini ya Uongozi wangu na wajumbe wa TESDO BW.Seifu Kazuge,Cassian Puis na Mansoor Juma tangu tarehe 21/05/2012 ofisini makao makuu Tesdo.Aidha mikamati ya kujitolea ilifanywa na majukumu kugawiwa wajumbe wote.
TESDO OFISIN-viongozi kwakiratibu Seminar
Cassian Puis alijitolea kutengeneza tangazo kwa gharama zake-TSH.100,000/=,Katibu Mtendaji nilisimamia mambo yote yahusuyo Stationaries na Seif alifuatilia Ukumbi na maandalizi yake.wajumbe wengine wakafanya zoezi ya uhamasishaji mahudhurio.
SEMINA KUFANYIKA
Mnamo tarehe 26/05/2012 saa 2.00 asubuhi wajumbe NA VIONGOZI WA TESDO waliwasili eneo la ukumbi wa SAUT/mihayo school.
Vongozi TESDO wakisubiri wajumbe wa semina-UKUMBI WA CHUO CHA SAUT TABORA
Wajumbe wa semina walitarajiwa kuwa wengi sana kwa matangazo tuliokuwa tumetoa kwa vyombo vya Redio lakini haikuwa hivyo kinyume na matarajio yetu.Lakini imani yetu ni kuwa mwanzo mgumu na harakati hizi za kubadili mitazamo na ujanja wa kutumia fursa zinazopatikana ni suala la lazima.Hali ilikuwa hivi
Ni wajumbe wachache sana aliohudhuria semina hii
Lakini TESDO na viongozi ake wanaamini katika harakati ya kubadili tabia na mtazamo si jambo lahisi kiasi hicho;hivyo basi kwa kuzingatia rasilimali zilizotumika kuandaa ukumbi ilitupasa kufanya semina kwa wajumbe hawa na kufikisha lengo ili tuwe na wachache wenye nguvu na sio wingi wa povu la sabuni. Semina ikaanzaa;mada zikaanza tolewa.
Mada ya kwanza: Nafasi ya wasomi kusaidia maendeleo ya Mkoa wa Tabora
Wawasilishaji mada TESDO MAKAO MAKUU-aliesimama ni SEIF(kushoto),katikati M.Mapalala na (kulia) ni mjumbe Cassian Pius.
Pamoja na hayo;mada zote zilizopangwa kuhudhurihshwa zilitolewa na wajumbe wakapata kile walicho tarajia kupata.
Mada ya pili: MFUMO WA ELIMU TANZANIA NA FURSA ZA KIELIMU.
Mwasilishaji: Mohamed Mapalala
Mada ya Tatu: MAISHA YA CHUO NA CHANGAMOTO ZAKE
Mwasilishaji: Mansoor Juma
VIBURUDISHO NA VINYWAJI :
Pamoja na umaskini tuliokuwa nao haikuwa ngumu kufanya makoo yetu safii kwa kutoa mada na kuuliza maswali;
wajumbe wakisikiliza mada na kuburudika soda na maji
Meza ya wawezeshaji –TESDO MAKAO MAKUU
MCHANGANUO WA MATUMIZI
Tulipata fedha toka vyanzo vifuatavyo;
- Meya manispaa-50,000/=
- Cassian-100,000/=
- Mapalala 50,000/=
- Utawala SAUT Tabora -200,000/=
JUMLA:400,000/=
Mchanganuo huu ni kwa fedha (gharama) ila Fedha taslimu ilikuwa ni TSH.50,000/= tu.Zinginezo ni huduma zilizotolewa na wahusika kwa gharama hio.
MATUMIZI
Kutengeneza JINGO(TANGAZO)-100,000/=
- Kulitangaza Tangazo-30,000/=
- Kutoa copy na kuandaa semina papers-50,000/=
- Ukumbi-200,000/=
- Soda na maji 10,000/=
MWISHO
Tunatoa tena shukrani kwa wadau wa maendeleo kufanikisha hili kwa asilimia hii ndogo.Aidha tuna amini kwa wakati mwingine tutaweza zaidi.
Taarifa hii imeandaliwa na:
KATIBU MTENDAJI –TESDO
0715449745
mapalala04@gmail.com